UNAWEZA KUJIAMINI BILA KUONESHA DHARAU?
Mchezo wa Masumbwi, ni moja kati ya michezo inayotaka kujiamini pasipo kuonyesha dharau ili kuweza kumshinda mpinzani wako Kuna mstari mwembamba sana unaotenganisha maana ya neno kujivuna na kujiamini. Ni vigumu sana kumtofautisha mtu anayejivuna au kwa Kiswahili kingine mtu ‘anayejisikia’ na mtu anayejiamini. Lakini hakuna mtu anayependa kufuatana na mtu anayejisikia, hata watu wanajisikia wanakubali kuwa wanachukia majivuno. Tatizo lililopo katika suala hili ni kwamba watu wengi wanapata tabu sana kutofautisha watu hawa wawili. Mtu anahitaji kujiamini kiasi na siyo kupita kiasi kwa kila jambo. Hivyo mtu anayejiamini ana sifa zipi? Unaweza kumuelezea vipi mtu mwenye majivuno? Na mwisho kabisa, lakini ni muhimu, mtu anaweza je kuwa unajiamini tu bila kujikuta umeingia katika mtego wa watu wenye majivuno? Zijue tofauti hizo: MTU MWENYE MAJIVUNO Mtu mwenye majivuno au anayejisikia, siku zote hujiona ndiye bora. Siku zote hujifanya anajua kitu kilicho bora kwa wengine. Anapofa...