Posts

Showing posts from July, 2025

Rahisi kupata na rahisi kukosa!

Kanuni ya kupata unachohitaji maishani ni nguvu iliyopo hapa ulimwenguni kwa ajili ya kuvuta kitu fulani au kulivuta jambo fulani, huzikutanisha nguvu zifanano kwa njia hii ya mvutano. Kanuni hii inajidhihirisha kupitia nguvu ya uumbaji popote pale na kwa namna mbalimbali. Hata kanuni maarufu ya kisayansi ya law of gravity ambayo ndiyo asili ya uundwaji wa ndege ni moja ya kanuni ya kupata unachohitaji maishani. Kanuni ya kupata unachohitaji maishani huvuta mawazo, watu, hali, n.k. Kanuni ya kupata unachohitaji maishani hujidhihirisha katika mawazo yako na kuyavuta na kuyaleta mawazo yanayoshabihiana na mawazo yako; watu wanaofikiri kama wewe, na mambo kama hayo. Kanuni hii ndiyo inayowaunganisha watu wenye mahitaji na utashi unaofanana, ambao wako katika makundi mbalimbali – kama wanasiasa, timu za michezo, wapenzi na mengineyo. Ili kanuni hii iweze kufanya kazi, huhitaji kuwa na uhakika kamili. Kuamua kujenga taswira mawazoni; pia kwa kurudiarudia maneno ya aina fulani mara kwa mara....