Rahisi kupata na rahisi kukosa!
Kanuni ya kupata unachohitaji maishani ni nguvu iliyopo hapa ulimwenguni kwa ajili ya kuvuta kitu fulani au kulivuta jambo fulani, huzikutanisha nguvu zifanano kwa njia hii ya mvutano.
Kanuni hii inajidhihirisha kupitia nguvu ya uumbaji popote pale na kwa namna mbalimbali.
Hata kanuni maarufu ya kisayansi ya law of gravity ambayo ndiyo asili ya uundwaji wa ndege ni moja ya kanuni ya kupata unachohitaji maishani.
Kanuni ya kupata unachohitaji maishani huvuta mawazo, watu, hali, n.k.
Kanuni ya kupata unachohitaji maishani hujidhihirisha katika mawazo yako na kuyavuta na kuyaleta mawazo yanayoshabihiana na mawazo yako; watu wanaofikiri kama wewe, na mambo kama hayo.
Kanuni hii ndiyo inayowaunganisha watu wenye mahitaji na utashi unaofanana, ambao wako katika makundi mbalimbali – kama wanasiasa, timu za michezo, wapenzi na mengineyo.
Ili kanuni hii iweze kufanya kazi, huhitaji kuwa na uhakika kamili.
Kuamua kujenga taswira mawazoni; pia kwa kurudiarudia maneno ya aina fulani mara kwa mara. Kwa kufanya hivi utaleta katika maisha yako kile ulichokijengea taswira mawazoni au ambacho umekuwa ukikitamka mara kwa mara.
Hapa chini nimekuletea maelezo zaidi kuhusu kanuni hii na inavyojidhihirisha:
Kanuni hii ni udhihirisho wa nguvu ya uumbaji ya ulimwengu.
Ni kutokana na kanuni hii kitu chochote huumbwa: kikundi cha nyota, sayari, vyuma, miamba na hata miti, wanyama na watu.
Kanuni hii inatufundisha kwamba, vitu vinavyofanana huvutana.
Mawazo huvuta hali inayofanana na mawazo hayo. Unapata kile unachokifikiria.
Unakipata katika maisha yako kile ambacho akili na mawazo yako yanakizingatia. Mawazo chanya huvuta matokeo chanya. Mawazo hasi huvuta matokeo hasi.
Kama muda wako mwingi unafikiria matatizo na vikwazo ni mambo hayo hayo ndiyo utakayoyapewa.
Kama hufikiri na kutegemea mafanikio bila kuruhusu hofu kuingia mawazoni mwako, hatimaye utapata mafanikio.
Haitoshi kuwa na matumaini ya kupata kitu, unatakiwa kuwa na uchu mkubwa wa kukipata huku ukiamini kabisa kuwa utakipata, na ukikumbatia jambo hilo litakoea kuwa kweli.
Ili mawazo yako yatokee na kuwa ukweli, huna budi kuyarudia mara kwa mara huku ukiyongeza hisia, utashi na nia.
Mawazo yako ni chimbuko la jinsi utakavyoishi.
Kanuni hii inatumika na kila mtu, ingawa mara nyingi bila kutambua. Kuujaza ubongo kwa hofu na wasiwasi kila wakati huleta mawazo, matukio na watu kukuthibitishia maneno na mawazo yako.
Ukiujaza ubongo na mawazo ya furaha utavuta furaha katika maisha yako.
Comments
Post a Comment