Tunda linavyoweza kukurudisha katika ujana
Tumekuwa tukiulizwa sana swali hili linalohusu matunda. Wasomaji wetu wengi wamekuwa wakitaka kujua namna nzuri ya kula, lakini wengi wakiwa tayari wanajua kwamba matunda na mbogamboga ndiyo vyakula vinavyomfaa zaidi binadamu, wamekuwa wakitaka kujua namna nzuri ya kula matunda.
Wengi wetu tunaposikia kula matunda tunadhani ni kuyatafuta au kuyanunua na kuyakatakata halafu kuyatumbukiza mdomoni, kuyatafuna na kuyameza. Hivyo kwa kweli siyo, kwani kuna utaratibu unaofaa wa ulaji wa matunda. Tumeona litakuwa ni jambo la busara iwapo tutakuelezea namna bora ya kula matunda, ili upate faida zaidi ya ulaji huo.
Kuna watu wanaokula matunda baada ya chakula. Hili ni kosa kubwa sana. Matunda yanapaswa kuliwa au kunywa kwenye tumbo tupu, yaani wakati mtu akiwa na njaa. Mtu ambaye anaweza kula tunda kwenye tumbo tupu na kabla ya mlo mkuu, anaweza kufaidika zaidi na ulaji huo wa matunda kuliko yule anayefanya kinyume chake.
Hebu tuchukulie kwamba ni asubuhi ambapo umekula vipande viwili vya mkate na chai na baada ya hapo ukachukua tunda na kulila. Tunda kwa kawaida linatakiwa kupita kwenye utumbo mkubwa na kwenda moja kwa moja kwenye utumbo mdogo, lakini hapa sasa zoezi kama hili halitawezekana. Ina maana kwamba, tunda litakuwa limezuiwa kwenda kwenye utumbo huo.
Wakati huo huo chakula chote kilicholiwa kinaanza kuoza na kuvunda, ambapo hugeuzwa kuwa asidi. Pale tunda lililoliwa linapokutana na chakula kwenye utumbo mkubwa, ambapo pia hapa kuna kemikali za kusagia chakula, mkururo huo huanza kuharibika. Ni wazi umeshawahi kusikia watu wakisema kwamba, wanapokula tunda na kula chakula huwa wanapiga sana mbweu au kucheua kwa fujo. Hapa ni kwamba tunda limesababisha tunda kuharibika kwa chakula.
Kuna wengine ambao hulalamika kwamba wanapokula chakula na baadaye kula tunda kama ndizi hujikuta wakitamani kukimbilia chooni. Wengine hulalamika kwamba wanahisi tumbo kujaa au kuvimbia. Hii haiji tu, bali ni tunda hilo lililoliwa baada ya mlo linafanya vitu vyake.
Hali kama hizi haziwezi kutokea kama mtu anaweza kula tunda kabla ya mlo. Kwani kufanya hivyo, hakuwezi kusababisha tunda kuchanganyika na vyakula ambavyo vimeanza kufanyiwa kazi. Watu ambao wanakula matunda kwa utaratibu mzuri wako kwenye nafasi kubwa na nzuri ya kujiepusha na vipara, hasira za haraka, alama nyeusi chini ya macho na matatizo mengine ya kimwili.
Kuna wengine ambao huogopa au hudhani ni vibaya kula tunda wakati tumboni hakuna chakula, kwa sababu matunda hayo yana asidi, hasa matunda ya jamii ya machungwa. Lakini kufuatana na maelezo ya daktari Herbert Shelton ambaye amefanya utafiti wa kutosha suala hili, hii siyo kweli. Siyo kweli kwa sababu, kwa maelezo yake ni kwamba tunda lolote linapoingia tumboni hubadilishwa na kuwa alkali.
Inaelezwa kwamba kama mtu akimudu kula matunda katika utaratibu unaokubalika, anajiweka kwenye nafasi nzuri sana ya kuwa na uzuri wa asili, kushikilia maisha marefu zaidi, kuwa na afya bora, nguvu, kuwa na uzito unaokubalika kiafya na faida nyingine kama zilivyobainishwa awali.
Unywaji wa juisi za madukani, yaani ambazo zimetengenezwa viwandani na kuhifadhiwa kwenye makopo au maboksi, unakatazwa. Juisi hizi zimewekewa dawa za kufanya zisiharibike, zimewekewa rangi ya vyakula na hizi zote ni kemikali ambazo zina athari
kwenye mwili. Lakini pia katika uandaaji inawezekana juisi hizi hupitia joto fulani kiwandani. Juisi ikishapashwa moto na virutubisho vyake navyo hupotea. Kwa hiyo, anachopata mnywaji hapa ni harufu ya juisi na siyo thamani ya virutubisho.
Kama mtu anakunywa juisi anashauriwa kunywa polepole, ili juisi iweze kuchanganyika na mate kabla hajaimeza. Ni muhimu juisi kuchanganyika na mate kabla haijaenda tumboni.
Ili kuthibitisha kwamba matunda ni chakula muhimu na chenye nguvu kubwa kuliko unavyofahamu, hebu jaribu zoezi hili. Hili ni zoezi la kufunga kwa kutumia juisi na matunda. Kinachofanyika ni mtu kunywa juisi na kula matunda bila kitu kingine chochote kwa muda wa siku tatu.
Kwa siku hizo tatu mtu anatakiva kula matunda ya aina mbalimbali ambayo inabidi yatengenezwe kwa mitindo mbalimbali, ikiwaemo juisi. Bila shaka kwa mgeni wa matunda na mtu anayependa kula sana inaweza kuwa ngumu. Lakini mtu akimudu kufunga kwa siku hizo tatu, ni wazi atashangaa, kwani rafiki zake ni lazima watamuuliza ‘siku hizi unakula nini mbona unang’ara sana.’ Si vibaya kujaribu kwani haiuwi.

Comments
Post a Comment